Fidstyle Friday Week 11 with ROMA

Rhymes Of Magical Attraction, aka ROMA, ndani ya Fidstyle Friday. Nadhani wengi hawatashikwa na mshtuko watakapoona na kusikia vijana wadogo (yaani, watoto) wakichana nyimbo za zake mitaani — mfano mzuri ni kijana huyu kutoka Ifakara.

Lakini, kama kawaida, ushairi wa tungo za hip hop unabeba mistari mizito, kwa mfano, “Nilikuwa nina ndoto za kuwa pastor, [ila] zikayeyuka nilipopuliziwa moshi wa bangi.” Ni mstari unaoweza kuchukuliwa kama ulivyo, kwa wepesi tu, lakini unabeba ujumbe mzito. Wiki hii ROMA anaelezea alikuwa anamaanisha nini (ukitaka kujielemisha zaidi kuhusu mistari kama hiyo basi bofya hapa)…

Kilio cha wasanii kinajirudia. Miradi au kazi zao zimekamilika lakini mfumo wa usambazaji unawaangusha. Lini wasanii wataanza kufaidika ipasavyo?

Tovuti na kurasa nyingine kuhusu ROMA na Tongwe Records:

2011-10-27T18:00:40+00:00October 22nd, 2011|Featured, Fidstyle Friday|2 Comments

2 Comments

  1. KELVI KITOSI October 27, 2011 at 6:35 pm

    ROMA AMETISHA BAAAAB, SEMA ANABEEF NA WANA WA KASKAZINI? KWENYE MISTARI YAO MYEUSI NAIPAKA CAROLITE HAPO KUNA UTRATRA

  2. alec margason November 2, 2011 at 7:22 pm

    Ngosha kama Host toka jiji la Miamba na ROMA mpare wa milimiani ila ni mtoto wa kitanga_bonge la comb’enwei Bg up Fid najua ni harakati kuanzia u_tube to tv station,then umeanza na studio utafika kushuhudia battle za mtaan.
    ONE

Comments are closed.