Siri ya Mchezo

Fid-q-siri-ya-mchezo

Today Fid-Q release his 3rd single from his anticipated album, KitaaOLOJIA titles Siri ya Mchezo featuring Juma Nature on the hook. The track is produced by Ben Mwamba.

Track can be downloaded here: Siri ya Mchezo-Fid Q ft Juma Nature.mp3

SIRI YA MCHEZO LYRICS

Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na  umuhimu kihivyo… stimu  zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../  sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop/
Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa  #teamMabiiitoz  /
Achana na  power window.. sijui  rimz za dimpoz/
haileti bingo, mshiko?  Star ishi simple/   sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui  kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa  ukuone hauna ishu/
ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za  harakati ni ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/  na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji  kama  Kubanda eti unachana kigumu/  kisa  track ikivuma sana kwenye chati  haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA../  baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../  najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na wakinitisha najihami../  inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
‘’Pole MAPROSOO’’ ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni  wahuni  hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../  huo ni utumwa pia/Unafanya  vijana  wanaumia../
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..

 

 

CHORUS:  ( Juma Nature )

Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2
Siri ya mchezo naijua  mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2

 

 

VERSE 2:

Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma/ wakati SIASA kila mara ukiwa unang’ara ujue kuna.. kinara/ anayeunda msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/ KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/
tuone kufuru za wenye hela/
TANZANIA ni ‘  demu wa mtungo ‘ wanamuiita CHA WOOTE/’’ HANGOVER .. ‘’anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote/
Mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake/ ‘’na  gari bovu..’’  halisukumwi kwa kukaa ndani yake/
MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza../  je  Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza? /
hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion/
na daily tunafeli sababu ya  POLITICAL institutions/
CIVILIZATION  imeadvance sasa wanatuua economically../
hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free/
Kuusaka ukweli  ni  sawa na kumenya kitunguu/
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/
Ukishafika kwenye kiini  niambie nini utagundua..?
zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka/
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA/
Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????

2018-08-16T08:42:04+00:00October 18th, 2013|Featured, News|24 Comments

24 Comments

 1. mateo October 18, 2013 at 6:19 pm

  tishaa mbaya fid q the best MC bongo hakunaga miaka yote

 2. Selestine George October 18, 2013 at 6:37 pm

  Bro we mkali daima hujawah niangusha mkali wangu ndude ya maana

 3. mahmoud October 18, 2013 at 6:54 pm

  kama fid q hakuna tz.huchoki na hautoi bubble gum music.big up xana.

 4. Sucre October 18, 2013 at 7:44 pm

  Goddamn it! You’re a blessed talent! You’re fuckin’ awesome man, very lyrically stable. You were born to do this thing. I’m grateful to see you and Sir Nature still got this shit. Good job indeed.

 5. ANGEDIZZLE October 18, 2013 at 8:30 pm

  best rapper alive

 6. jackson sunford October 18, 2013 at 8:46 pm

  Aseee Am a big fun of FId Q he amazing writer and rapper Big up Bro you the reason we love HIP HOP today…..Nice Song broh we got much love for ya……

 7. Tumsiime Mujwauzi October 18, 2013 at 9:59 pm

  Babu kubwa mkuu Big up………

 8. mouc October 18, 2013 at 10:13 pm

  we call it hip hop thanx umeitendea haki>>>>>> TRUE ……..TRUE

 9. Victor Katunzi October 18, 2013 at 11:11 pm

  Excellent brother,, i dream to be you ONE DAY.

 10. Hamza 'Hamzeli' Mkundi. October 19, 2013 at 12:11 am

  Wewe umeibeba HIP HOP ya Bongo mabegani brah… I like dat song iko poa sana jamaa…

 11. hiphop fan October 19, 2013 at 4:01 am

  umetisha bro..love the way u’flow, lyrics zako ziko poa daima.

 12. robert October 19, 2013 at 4:29 am

  killng them

 13. Fadha October 19, 2013 at 4:38 am

  que si fantastique et félicitations frère …….. HIP HOP vit FID Q

 14. agnapu October 19, 2013 at 10:50 am

  massive lyrics. fresh production. waiting for the album!

 15. Jams October 19, 2013 at 12:48 pm

  NA USKIAPO SAUTI YANGU NISOME KWENYE MISTARI,,,,,,,,,,,,,,,,FID Q,,,,,MUCH RESPECT HADI NAUGUA

 16. Paul October 19, 2013 at 2:46 pm

  Aminia xana kaka ngosha…..

 17. Lenny October 19, 2013 at 3:15 pm

  Fid. Q ur the best
  I real appriciate ur music”
  Keep it up bro!!!!!

 18. Freeman October 19, 2013 at 6:58 pm

  Hot!!! Fire!!! And i havent even listened to it yet.

 19. edger olomi October 19, 2013 at 7:48 pm

  man track ipo nga ile laana.big up bro

 20. Pius John October 20, 2013 at 3:35 am

  ebwana ngoma hii ni nouma mzazi

 21. valencie peter October 20, 2013 at 6:29 am

  u the best Ngoshaaa
  #CheusiDawa4eva

 22. shangwe October 20, 2013 at 6:46 am

  K2JyyoS5rzbs -WIMBO SIO MKALI KIVILE MICHANO ILE ILE FLOW ILE ILE IDEA ZILE ZILE HAKUNA IDEA MPYA KAMA SIHITAJI MARAFIKI ILIVYOKUWA..HAPO ANAENDELEZA TAMBO NA MAJIGAMBO

 23. Siri ya Mchezo | SportSquare October 22, 2013 at 10:13 am

  […] Siri ya Mchezo […]

 24. Kuchaga October 31, 2013 at 11:18 am

  Fid,u make me happy bro! Nakukubali sn

Comments are closed.